MAOMBI YA VYETI VYA KUZALIWA, UHAKIKI NA MAREKEBISHO YA VYETI KUPITIA RITA

MAOMBI YA VYETI VYA KUZALIWA, UHAKIKI NA MAREKEBISHO YA VYETI KUPITIA RITA
Wananchi wote mnaarifiwa kuwa sasa mnaweza kuwasilisha taarifa zenu kwa ajili ya kuombewa huduma za Vizazi kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ikiwemo:
· Kuomba Cheti cha Kuzaliwa
· Kuhakiki Cheti cha Kuzaliwa au Kifo
· Kubadilisha Cheti cha Zamani kuwa Cheti Kipya cha Kielektroniki
· Kuomba Marekebisho ya Taarifa kwenye Cheti cha Kuzaliwa
📌 NAMNA YA KUWASILISHA TAARIFA ZAKO
Ili kuanza mchakato, tafadhali jaza fomu kupitia link ifuatayo kwa usahihi:
👉 https://forms.gle/3PTxeoWZ1ZiiYVF59
Taarifa utakazowasilisha zitatumika kukusaidia kuomba au kufuatilia huduma husika kupitia mfumo wa RITA (eRITA).
UTANGULIZI KUHUSU RITA NA USAJILI WA VIZAZI
RITA ni chombo cha Serikali kilichokasimiwa jukumu la msingi la kusajili Matukio Muhimu ya Binadamu, ikiwemo vizazi na vifo, kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo, Sura ya 108, inayotaka matukio yote yanayotokea Tanzania Bara kusajiliwa kisheria.
UMUHIMU WA USAJILI WA VIZAZI
Usajili wa vizazi una faida kubwa kwa mtu binafsi na kwa Taifa kwa ujumla, ikiwemo:
1. Kupata Cheti cha Kuzaliwa kinachomruhusu mhusika kupata haki za kijamii kama elimu, ajira (serikali na binafsi), na kujiunga na vyombo vya ulinzi na usalama.
2. Kuwezesha kupata Hati ya Kusafiria, ambapo taarifa za wazazi, tarehe na mahali pa kuzaliwa hutumika kuthibitisha utambulisho.
3. Kuthibitisha umri wa mtu kwa madhumuni ya utekelezaji wa sheria mbalimbali (ajira, ndoa, uchaguzi n.k.).
4. Kuwezesha mtoto kupata haki ya uraia, endapo mzazi mmoja ni Mtanzania.
5. Kusaidia Serikali kupanga mipango sahihi ya maendeleo na kijamii kulingana na takwimu za idadi ya watu.
6. Kusaidia Serikali kufahamu viwango vya uzazi (fertility rate).
7. Kuwezesha warithi kupata stahili za marehemu kama mirathi, bima na mafao mbalimbali.
8. Kuwezesha watoto yatima kupata huduma za kijamii na misaada.
UMUHIMU WA USAJILI KATIKA MIFUMO MINGINE YA SERIKALI
Usajili wa vizazi unaunganishwa na mifumo mingine muhimu, ikiwemo:
· NIDA – Utambuzi wa uraia au ugeni
· Daftari la Wapiga Kura – Uthibitisho wa umri wa kupiga kura
· Hati za Kusafiria – Uthibitisho wa mahali pa kuzaliwa na wazazi
· Sensa ya Watu na Makazi – Kupunguza gharama za zoezi la sense
HUDUMA ZA RITA KUPITIA MFUMO WA eRITA
Huduma za usajili wa vizazi na vifo zinapatikana kupitia mfumo wa kielektroniki (eRITA) unaomwezesha mwombaji kupata huduma kwa urahisi, usalama na kwa gharama nafuu.
🌐 Tovuti: www.rita.go.tz → chagua menyu ya eRITA
MAOMBI YA CHETI CHA KUZALIWA
Mahali pa Usajili
1. Kituo cha tiba au ngazi ya kitongoji (ndani ya siku 90)
2. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya (usajili wa kuchelewa)
3. Kupitia mtandao (eRITA)
Mahitaji ya Jumla
Mwombaji aambatishe hati mbili kati ya zifuatazo:
· Kadi ya Kliniki ya Mama au Mtoto
· Tangazo la Kuzaliwa
· Cheti cha Ubatizo
· Vyeti vya shule
· Pasi ya kusafiria / Kadi ya mpiga kura
Pamoja na kitambulisho cha mzazi/mlezi (ikiwa wazazi wapo hai).
ADA MUHIMU
· Usajili wa kawaida: Tsh 7,000
· Usajili wa kuchelewa chini ya miaka 10: Tsh 8,000
· Zaidi ya miaka 10: Tsh 20,000
· Uhakiki wa cheti: Tsh 6,000
· Kubadilisha cheti cha zamani kuwa kipya: Tsh 8,000
· Marekebisho ya cheti: Tsh 13,000
Utapewa Control Number kutoka RITA na kulipia.
HUDUMA ZA MAREKEBISHO YA CHETI CHA KUZALIWA
Marekebisho hufanyika kwa kuwasilisha barua ya maombi, cheti halisi, viambatanisho vya uthibitisho na kulipia ada husika. Huduma hii kwa sasa hufanyika kwa kufika ofisi za RITA Makao Makuu au Wilaya.
HITIMISHO
Wananchi wote mnaombwa kujaza fomu kupitia link iliyotolewa ili kuwezesha ukusanyaji wa taarifa zenu na kusaidia mchakato wa maombi yenu ya vyeti na marekebisho kufanyika kwa ufanisi.
📌 Link ya Kutuma Taarifa:
👉 https://forms.gle/3PTxeoWZ1ZiiYVF59
Kwa usahihi wa huduma, tafadhali hakikisha taarifa zote unazowasilisha ni sahihi na kamili.
